Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wasema kipindukipindu bado tishio DRC

UM wasema kipindukipindu bado tishio DRC

Umoja wa Mataifa umesema kwamba tatizo la ugonjwa wa kipindupindu ambao ulizuka hivi karibuni katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, unaendelea kuwa tishio  kubwa na umeanza kusambaa katika nchi za jirani pia.

Kulingana na takwimu zilizotolewa na shirika la afya ulimwenguni WHO, watu zaidi ya 3,896 tayari wamekubwa na ugonjwa huo tangu ulipozuka mwezi wa March mwaka huu.Kumekuwa na juhudi kadhaa toka kwa jumuiya za kimataifa ambazo zimeongeza nguvu kukabiliana na kusambaa kwa ugonjwa huo.Hadi kufikia Julai 20 idadi ya watu waliofariki dunia ilifikia 265.