Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya uhaba wa chakula yazidi kuwa mbaya pembe ya Afrika

Hali ya uhaba wa chakula yazidi kuwa mbaya pembe ya Afrika

Wataalamu kwenye Umoja wa Mataifa wameonya kuwa huenda mamilioni ya watu wakakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula nchini Somalia na pembe ya Afrika ikiwa jamii ya kimataifa haitaingilia kati kuweza kukabilina na hali hiyo.Shamsul Bari mtaalamu wa masuala ya haki za binadamu nchini Somalia na Olivier de Schutter ambaye ni mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kuwa na chakula wanasema kuwa jamii ya kimataifa ina fedha na uwezo wa kuzuia janga hilo la njaa.

Naye mkuu wa haki za binamu kwenye Umoja wa Mataifa Antonio Gutteres aliyetembelea Ethiopia na Kenya ametoa wito kutolewa kwa misaada ya kimataifa kusadia kukabiliana na hali kwenye pembe ya Afrika. Akiongea alipotembea kambi ya Daadab nchini Kenya Gutteres amesema kuwa Somalia imakabiliwa na janga kubwa zaidi duniani. Immanuel Nyabera ni msemaji wa UNHCR nchini Kenya.

(SAUTI YA IMMANUEL NYABERA)