Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujenzi mpya wa Haiti uzingatie haki za binadamu-UM

Ujenzi mpya wa Haiti uzingatie haki za binadamu-UM

Umoja wa Mataifa umesema kuwa shughuli za kulijenga upya taifa la Haiti ambalo liliharibiwa vibaya kutokana na majanga ya kimaumbile, lazima zienda sambamba na uheshimuji wa haki za binadamu.Sura na mwonekano wa taifa la Haiti iliharibiwa vibaya kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba nchi hiyo iliyoko pembezoni mwa bahari ya Pasifiki.

Kwa mujibu wa Naibu kamisha wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya haki za  binadamu, Kyung-wha Kang, lazima kuhakikisha kuwa wakati huu wa ujenzi mpya hakuna makundi yanayowekwa kando.Ametaka miradi na mipango yenye shabaya ya kulijenga upya taifa hilo inashilikisha makundi yote ya watu na kusisitiza kuwa saula uwazi na ukweli ndiyo ngao muhimu itayokaribisha matumaini kwa wote.Afisa huyo amekalimisha ziara yake ya siku tano kutembelea maeneo mbalimbali ya nchi hiyo yaliyoharibiwa na tetemeko hilo la ardhi.