Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu zaidi wanahitaji misaada Sudan Kusini : OCHA

Watu zaidi wanahitaji misaada Sudan Kusini : OCHA

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA linasema kuwa asilimia kubwa ya wenyeji milioni 1.4 katika jimbo la Kordofan Kusini wanahitaji misaada ya kibinadamu na hadi sasa watu 75,000 wamekimbia makwao.

OCHA inasema kuwa hali katika eneo la Upper Nile inasalia kuwa mbaya huku mizozo ya kijamii ikizidi kuongezeka. Kwa upande wake shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa kuhama kwa watu kutoka makwao linasalia kuwa tatizo kubwa hata kama eneo la Sudan Kusini linatangazwa huru tarehe 9 mwezi huu.

(SAUTI YA MAUREEN KOECH)