UNICEF na kamati ya olimpiki waungana kupinga kutengwa wenye ulemavu

27 Juni 2011

UNICEF na olimpiki maalum waungana kuangamiza kutengwa kwa watoto walio na ulemavu

Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF pamoja na olimpiki maalum za msimu wa joto zitakazoandaliwa mjini Athens wametia sahihi makubaliano ya kuwepo ushirikiano katika kutetea haki , hadhi na kujumuishwa kwa watoto walio na ule kwenye mashindano maalum.

Mwenyekiti na mkurugenzi mkuu wa mashindano hayo Timothy Shriver pamoja na mkurugezni wa UNICEF Anthony Lake walihaidiana kuimarisha ushirikiano wao na kufanya kazi kwa pamoja ili kuangamiza vizingiti vya kijamii na vya kimaumbile vinavyowazuia watoto walemavu kushiriki mashindano hayo.

Watoto walemavu mara nyingi huwa wanatengwa na kukataliwa na pia hunyimwa huduma muhimu zikiwemo za kiafya, elimu na masuala mengine ya kijamii.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter