Wanaume Zanzibar waongeze washiriki katika vita dhidi ya ukimwi:Duni

24 Juni 2011

Vita dhidi ya ukimwi na hususani maambukizi mapya ni suala linalopigiwa upatu sana na Umoja wa Mataifa na mashirikia yake likiwemo la kupambana na ukimwi UNAIDS, la afya WHO, la idadi ya watu UNFPA, la watoto UNICEF na wadau wengine wa kitaifa na kimataifa, yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali yaani NGO’s.

Mapema mwezi huu Umoja wa mataifa uliitisha mkutano hapa New York kuitathimini hatua zilizopigwa na nchi wanachama katika vita dhidi ya ukimwi tangu kuzuka kwa gonjwa hilo yapata miaka 30 iliyopita.

Kuna baadhi ya nchi zimepiga hatua kubwa na zingine bado zinajikongoja, lakini nia yao ni moja kuhakikisha kuna maambukizi mapya sufuri, vifo vya ukimwi sufuri na maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa motto sufuri. Na kama alivyosisitiza Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon vita dhidi ya ukimwi si vya mtu au taifa moja ni vita vya duniania nzima.

Visiwani Zanzibar wanakubaliana na wito huo na waziri wa afya wa visiwa hivyo Juma Duni Haji anasema hasa wanaume wanatakiwa kuongeza ushiriki wao katika vita hivyo.

Ametanabaisha hayo aliopozungumza na mku wa idhaa hii Flora Nducha kuhusu juhudi zilizopigwa na serikali yake katika vita dhidi ya ukimwi ugonjwa uliobainika kwa mara ya kwanza Tanzania miaka 28 iliyopita.

(MAKALA FLORA NDUCHA NA JUMA DUNI)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter