Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka uchunguzi zaidi juu ya taarifa za kuendelea kuzama boti za wahamiaji Afrika ya Kati

UM wataka uchunguzi zaidi juu ya taarifa za kuendelea kuzama boti za wahamiaji Afrika ya Kati

 Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limetoa mwito wa kufanyika kwa uchunguzi wa haraka dhidi ya tukio la kuzama maji kwa boti moja iliyokuwa imebeba wahamiaji ambao walikuwa wakikimbia hali mbaya ya kisiasa katika eneo la Afrika ya kaskazini.

Katika miezi ya karibuni kumekuwa na ripoti za mara kwa mara zinazonyesha kuwepo kwa matukio ya kuzama kwa boti kwenye bahari ya Mediterranean ambako kunawahusisha wale wanaokimbia hali mbaya ya kisiasa nchini Libya.

 Afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa hivi karibuni alidai kuwa watu zaidi ya 600 walizama maji kwenye pwani ya Libya wakati boti yao waliyokuwa wakisafiria ilipovunjika.

Katika taarifa yake baraza hilo la haki za binadamu limeelezea masikitiko yake kutoka na matukio ya watu kuzama hasa zaidi la hivi karibuni ambapo wasafiri wanakadiriwa kufikia mia kadhaa walipoteza maisha kutokana na kuzama kwa chombo chao. Limetaka mamlaka kuanza uchunguzi juu ya ripoti hizo.