Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yataka dola milioni 160 kusaidia wahamiaji Libya

IOM yataka dola milioni 160 kusaidia wahamiaji Libya

Huku kukiwa hakuna dalili ya kukoma mapigano yanayoendelea sasa nchini Libya mamia kwa maelfu ya wakimbizi wameendelea kuondoka nchini humo jambo ambalo linazidisha haja ya hitajio la msaada wa dharura.

Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM limesema kuwa linahitaji kiasi cha  dola za kimarekani milioni 160 ili kuweza kuendelea kutoa msaada wa kuwaokoa wahamiaji hao ambao pia wapo kwenye hitajio kubwa la misaada ya kibinadamu.

Tangu kuzuka kwa machafuko hayo mwezi February mwaka huu , zaidi ya wahamiaji 410,000 wamekimbia kutoka nchini humo na kumesalia mamia kwa maeflu ya wahamiaji wengine ambao wanahitaji kuokolewa. Ili kuwafikia wahamiaji hao waliosalia shirika hili la uhamiaji limeendelea kutoa mwito kwa jumuiya za kimataifa kuchangisha mafungu ya fedha