Wanawake na watoto kubeba gharama za machafuko Libya:UNICEF

17 Juni 2011

Wanawake na watoto ndio watakaoathirika zaidi na kubeba gharama za machafuko nchini Libya endapo vita vitaendelea kwa muda mrefu na hawatalindwa limesema shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa mataifa UNICEF.

Shirika hilo linasema shule hazifanyikazi tena, wakati huduma muhimu za afya zikiwemo chanjo la kila msimu zimesitishwa kutokana na upungufu wa dawa. UNICEF pia imesema huduma za maji na usafi ambazo hazikuathirika na mapigano sasa zinakabiliwa na matatizo kutokana na upungufu wa vipuri na madawa ya kusafishia maji. Pierre Poupard ni mkuu wa timu ya dharura ya UNICEF nchini Libya.

(SAUTI YA PIERRE POUPARD)

UNICEF inasema mabomu ya ardhini na mabaki mengine ya silaha ambazo ambayo hazijaripuka pia ni tishio kubwa kwa maisha ya watoto nchini Libya.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter