Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ubaguzi watajwa kukita mizizi miongoni mwa jamii ya Roma

Ubaguzi watajwa kukita mizizi miongoni mwa jamii ya Roma

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya ubaguzi Githu Muigai amesema kuwa ubaguzi uliokita mizizi na ukosefu wa uvumilivu ni kati ya masuala yaliyo miongoni mwa watu wa jamii ya Roma barani Ulaya na watu waliozushwa hadhi barani Asia , Afrika na eneo la Mashariki ya Kati.

Akiwasilisha ripoti yake mbele ya baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa Muigai amesema kuwa waathiriwa wote wa mambo haya ni lazima wahakikishiwe usalama. Mjumbe huyo amesema kuwa ni bora kuchukua hatua zifaazo kupitia kwa njia za kisheria na kisiasa.

Muigai pia ametoa wito kwa serikali kutoa habari zinazohusiana na ubaguzi na pia ukusanyaji wa takwimu ili kuweza kuelewa idadi ya watu wanaoathirika na masuala haya.