Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji zaidi waondolewa Misrata kufuatua mashambulizi mapya

Wahamiaji zaidi waondolewa Misrata kufuatua mashambulizi mapya

Zaidi ya wahamiaji 200, wengi kutoka nchi za kusini mwa jangwa la sahara wakiwemo 30 waliojeruhiwa na kuokolewa na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kutoka mji wa Misrata nchini Libya, wamewasili salama mjini Benghazi hii leo. Wahamiaji hao walisafirishwa kwa kutumia meli ya IOM kufuatia mashambulizi mapya kwenye mji wa Misrata ambao umekuwa tulivu majuma machache yaliyopita. Wahamiaji hao waliokolewa kwenye oparesheni ya IOM iliyofadhiliwa na idara ya Marekani inayohusika na idadi ya watu , wakimbizi na wahamiaji wanaotoka Chad, Nigeria, Sudan na maeneo mengine mwa bara la Afrika. Jumbe Omari Jumbe ni afisa wa IOM:

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)