Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa UM kutathimini hali ya ukimwi duniani kuanza Juni 8 New York

Mkutano wa UM kutathimini hali ya ukimwi duniani kuanza Juni 8 New York

Kuanzia Juni 8 wiki ijayo viongozi wa dunia watakutana kwenye makao makuu ya Umoja wa mataifa hapa New York kujadili vita dhidi ya ukimwi, hatua zilizopigwa na nini kifanyike siku za usoni kuvishinda vita hivyo.

Ni miaka 30 tangu ukimwi ulipoikumba dunia na ni miaka 10 tangu baraza kuu la Umoja wa mataifa lilipofanya mkutano maalumu kuhusu ugonjwa wa ukimwi, sasa wakuu hao wa nchi na wawakilishi kutoka mataifa 30, mashirika ya kimataifa, jumuiya za kijamii na watu wanaoishi na virusi vya HIV watatathimini hatua walizopiga na hatua zipi zichukuliwe ikiwa ni pamoja na kutoka na azimio jipya.

Takwimu za shirika la afya duniani WHO na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na ukimwi UNAIDS zinaonyesha zaidi ya watu milioni 34 wanaishi na virusi vya HIV, milioni 6.6 wanapata dawa za kurefusha maisha ikiwa ni ongezeko la watu milioni 1.4 ikilinganishwa na mwaka 2009.

 Nimeketi chini na naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro ambaye kwa ushirikiano na mkurugenzi wa UNAIDS Michel Sidibe Ijumaa hii wamezindua ripoti ya kimataifa ya ukimwi itakayofanyiwa kazi kwenye mkutano huo, kwanza amenieleza kwanini ni muhimu Umoja wa Mataifa unafanya mkutano huu wiki ijayo.

(MAHOJIANO NA ASHA ROSE MIGIRO)