Machafuko yaliyozuka Yemen yasababisha vifo vya wakimbizi wawili

3 Juni 2011

Shirika la umoja wa mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR limesema kuwa limeanza kuingiwa na wasiwasi mkubwa juu ya hali ya mambo inavyojiri nchini Yemen katika wakati ambapo tayari kumeripotiwa kuuwawa kwa wakimbizi wawili katika machafuko yaliyofumuka upya.

Machafuko hayo yaliyozuka mwishoni mwa juma yakihusisha makundi ya kikabila yaliyopambana na vikosi vya serikali yametwaa maisha ya wakimbizi wawili raia wa Somalia.

Aidha ripoti zinasema kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la watu wanayoyakimbia makazi yao kutokana na kuzuka kwa machafuko hayo. Kumeshuhudia mamia ya familia

wakiondoka toka katika mji mkuu wa Sana’a na kuelekea upande wa kusini.Wakimbizi wengine walioko kwenye mji wa Hasaba ambao upo karibu kabisa na mjii mkuu wa Sana’a nao pia wamelazimika kukimbia

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud