Tunisia ina wakati mzuri wa kuangamiza mateso na dhuluma:Mendez

24 Mei 2011

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mateso Juan Mendez ameitaka serikali ya muda nchini Tunisia kutumia muda uliopo wa mabadiliko kuhakikisha kuwa mateso na dhuluma zingine hazitokea tena siku za usoni. Mendez anasema kuwa changamoto zinazokumba mabadiliko yanayoendelea nchini humo ni za kutisha.

Hata hivyo anasema kuwa raia wa Tunisia wanaishi wakiwa na matumaini ya maisha mema ya baadaye. Kulingana na Mendez serikali ya mpito ina wakati mgumu kuonyesha kuwajibika kwake kuitikia wito wa wananchi na kumaliza ukwepaji wa sheria uliokuwa tangu utawala uliopita ambapo dhuluma na mateso lilikuwa jambo la kawaida.

 Ameongeza kuwa hata kama dhuluma zimepungua vitendo vya mateso na dhuluma kutoka nyakati za uongozi wa rais Ben Ali vikiwemo vya kupigwa na kufungwa vinaonyesha tabia za zamani za polisi haziangamizwi kwa urahisi.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud