Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa baraza la afya duniani wakamilika leo mjini Geneva

Mkutano wa baraza la afya duniani wakamilika leo mjini Geneva

Ugonja wa kipindupindu umetajwa kama tisho kubwa kwa afya kwenye nchi nyingi huku tatizo hilo likiripotiwa kuongezeka. Haya ni kwa mujibu wa wajumbe kwenye mkutano wa baraza la afya duniani unaokamilika hii leo mjini Geneva. Wajumbe hao wamesema kuwa kuchukua hatua mwafaka za kiafya kama utafiti wa mapema, kuboresha mazingira, kuwepo kwa maji safi na kudumisha usafi kama baadhi ya hatua zinazostahili kuchukuliwa kukabialina na ugonjwa huo. Mkutano huo pia ulijadili njia za kuwalinda watoto kutokana na kuumia huku ripoti zikionyesha kuwa ajali za magari, Kuzama majini, kuchomwa, kuanguka na sumu huua zaidi ya watoto 830 kila mwaka. Wajumbe hao walikubaliana kuunga mkono jitihada kama vile sheria za matumizi ya vidhibiti mwendo, matumizi ya mikanda kwenye magari na kubuni vituo vya sumu kulingana na Dr David Meddings kutoka WHO.

(SAUTI YA DR DAVID MEDDINGS)