Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usalama bado mdogo Magharibi mwa Ivory Coast:UM

Usalama bado mdogo Magharibi mwa Ivory Coast:UM

Ripoti ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa maeneo kadhaa nchini Ivory Cost bado yanaandamwa na vitendo vya ghasia licha kwamba kwenye maeneo mengine ikiwemo mji mkuu wa Abidjan hali ya usalama inaendelea kuimarika na watu wanarejea kwenye shughuli zao za kawaida.

Maeneo yaliyotajwa kuwepo kwa hali ya ghasia ni yale yaliyopo upande wa magharibi ambako kunaarifiwa kwamba kumezuka mapigano ya hapa na pale .

Mkwamo wa kisiasa nchi humo ulifikia tamati mwezi uliopita baada rais aliyeng’ang’ania madaraka Laurent Gbagbo kutiwa nguvuni na vikosi vya hasimu wake Alassane Ouattara ambaye baadaye aliapishwa rasmi kuwa rais wa Ivory Cost.

Shirika la umoja wa mataifa la misaada ya kibinadamu OCHA limesema kuwa kutokana na mtawanyiko mkubwa wa watu uliojitokeza wakati wa machafuko, kunakwaza shughuli za kuziunganisha familia zilizokwenda mtawanyikoni.