UM waweza kupoteza hmashuhuri usipokaribisha mageuzi:Deiss

17 Mei 2011

Umoja wa Mataifa unakabiliwa na changamoto ya kupoteza heiba yake kwenye jukwaa la kimataifa kama kutaendelea kukosekana kufanyika kwa mabadiliko kwenye baraza la usalama.

Rais wa Baraza Kuu la umoja huo  Joseph Deiss ameongeza kusema kuwa ni jambo la kuchangaza kuona kwamba licha ya mijadala mbalimbali inayoendelea lakini hata hivyo hakuna mageuzi yaliyofanywa kwenye chombo hicho cha usalama.

Akizungumza kwenye kongamano linalojadilia umuhimu wa kufanyika mageuzi mjini Rome, rais huyo amesema kuwa baraza la usalama lazima likubali kuwa wakati umefika wa kufanyika mageuzi ili kwenda na mahitajio ya wakati pamoja na changamoto mpya zinazoendelea kuibuka.

Baraza hili la usalama linawachama 15 lakini wanachama 5 ndiyo wenye nguvu kutokana na kuwa na kura ya turufu.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter