Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni Siku ya Kimataifa ya Teknologia ya mawasiliano

Leo ni Siku ya Kimataifa ya Teknologia ya mawasiliano

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amesema kuwa kuboresha mawasiliano kutapunguza mwanya uliopo kati ya wasiopata na waopata habari hivyo kuboeresha maisha.

Kwenye ujumbe wakati wa maadhimiso ya siku ya kimataifa ya teknolojia ya mawasiliano yenye kauli mbiu maisha mema vijijini vilivyo na teknolojia ya mawasiliano, Ban amesema kuwa asilimia 70 ya watu bilioni 1.4 kwenye nchini maskini zaidi wanaishi vijijini akiongeza kuwa maewasiliano ya mtando yanaweza kusaidia katika kuafikiwa kwa malengo ya milenia ikiimaanisha kupungua kwa umaskini, utunzi wa mazingira , kuwaunga mkono akina mama na wasiobahatika kwenye jamii.