Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka rais mpya wa Haiti kuijenga upya nchi hiyo

UM wataka rais mpya wa Haiti kuijenga upya nchi hiyo

Umoja wa Mataifa umesema kuwa serikali mpya nchini Haiti ambayo imeingia madarakani kwa uchaguzi wa kidemokrasia inawajibu wa kuhakikisha kuwa machapuo mapya ya  kisiasa yanapewa nafasi ili hatimaye kujengwa upya taifa hilo ambalo limepitia kwenye vipindi kigumu katika miaka ya nyuma.

Rais mpya Michel Martelly aliapishwa rasmi mwishoni mwa juma katika sherehe zilizofanyika kwenye mji mkuu Port-au-Prince na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kimataifa akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migoro.

Rais huyo mpya ambaye kwenye duru la pili la uchaguzi wa mwezi wa March aliibuka mshindi amekabidhiwa madaraka hayo toka kwa mtangulizi wake René Préval.

Akitoa salama za Umoja wa Mataifa,Kiongozi wa ujumbe wa kulinda amani wa umoja huo nchini Haiti Bwana Martelly amesema kuwa kukamilika kwa amani kwa mchakato wa uchaguzi kunatoa ishara mpya kwamba wananchi wa Haiti sasa wamehitimu somo la ukomavu wa kidemokrasia.