UNECE yazindua mradi wa mazingira Moldova, Ukraine na Romania

12 Mei 2011

Ukraine, Moldova and Romania zimeanza rasmi mradi wa pamoja na Umoja wa Mataifa wa kuimarisha mazingira yaliyoaharibiwa na viwanda kwenye mto Danube.

Mradi huo unaongozwa na tume ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi kwa nchi za Ulaya. Shughuli za kiviwanda nchini Ukraine, Moldova na Romania kwenye mto Danube inaweka hatari ya kutokea kwa uchafuzi wa delta ya Danube.

Mradi huo una lengo la kuzuia ajali kwanza hasa usalama kwa vituo vya mafuta katika eneo hilo. Ujumbe wa nchi hizo tatu ulikutana mjini Kiev hii leo ili kuzindua rasmi mradi huo na shughuli zake kwa muda wa miaka miwili inayokuja hadi mwaka 2013.

Waliohudhuria walielezea umuhimu wa mradi huo kwa kila nchi na kutaka kuwe na ushirikino kati ya nchi hizo. Mradi huo unafadhiliw na wizara ya mazingira ya Ujerumani.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter