Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati ya UM inayohusika na habari yataka matumizi ya lugha nyingi

Kamati ya UM inayohusika na habari yataka matumizi ya lugha nyingi

Kamati ya Umoja wa Mataifa iliyotwikwa jukumu la kukagua sera za mawasiliano ya umma ya Umoja wa Mataifa na kutoa mwelekeo wa mawasiliano duniani imetoa wito kwa idara ya habari kuunga mkono matumizi ya lugha nyingi ili kuwafikia watu zaidi katika masuala tete ya kimataifa.

Kulingana na azimio la kamati hiyo ni kuwa malengo ya maendeleo ya milenia na athari za mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na hali ngumu ya uchuni duniani ni lazima yasalie kuwa malengo makuu kwenye kampeni.

Kamati hiyo imetoa wito kuwe na ufadhili zaidi ili kuiwesesha idara ya habari ya Umoja wa Mataifa kutumia lugha nyingi huku hati zote na zile zilizo kwenye mitandao zikiwa kwenye lugha sita rasmi zinazotumiwa kwenye Umoja wa Mataifa.