Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu zaidi ya 100 wauawa katika machafuko Syria

Watu zaidi ya 100 wauawa katika machafuko Syria

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa ameitaka serikali ya Syria kukomesha mara moja mauaji dhidi ya raia.

Kwa mujibu wa ofisi ya haki za binadamu zaidi ya watu 100 wameuawa mwishoni mwa wiki, wengine kukamatwa kama anavyofafanua msemaji wa ofisi ya haki za binadamu Rupert Colville

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

Katika mkutano na balozi wa Syria , kamishna mkuu Pillay amesema nchi hiyo imekaribisha ujumbe wa haki za binadamu kwenda kutathimini hali halisi lakini kwa masharti. Bi pillay amesema wanajiandaa kwenda na amerejea wito kwa serikali kukomesha machafuko na kutimiza ahadi ya kufanya uchunguzi wa mauaji ya wiki jana na siku zilizopita.