Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji zaidi ya 3000 wamehamishwa na IOM Libya

Wahamiaji zaidi ya 3000 wamehamishwa na IOM Libya

Zaidi ya wahamiaji 3100 wameshahamishwa kutoka eneo la mapigano la Misrata Libya kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM.

Shirika hilo linasema mapigano Misrata yanashika kasi hasa katika eneo la bandari ambako kuna wahamiaji wengi wanaosubiri kusafirishwa, na kuwaweka katika hatari ya mashambulizi ya maroketi na risasi. Watu wengi wanataka kuondoka mjini hapo kwa kutumia kila njia ikiwemo boti ndogo na IOM imekuwa ikiendesha shughuli hiyo.

Boti nyingine inatarajiwa kutia nanga Benghazi ikiwa na wahamiaji 1000 waliotolewa Misrata wengi wakiwa kutoka Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara, Bangladesh, Ufilipino, Pakistan, Misri, Algeria na Ukraine. Pia imebeba majeruhi 55 na maiti za waandishi habari wawili mpiga picha Tim Hetherington na Chris Hondros waliouawa jumanne katika shambulio Misrata.