Skip to main content

Usugu wa dawa dhidi ya maradhi lazima udhibitiwe:WHO

Usugu wa dawa dhidi ya maradhi lazima udhibitiwe:WHO

Shirika la afya dunianiWHO limeonya kwamba usugu wa dawa dhidi ya maradhi mbalimbali ni lazima udhibitiwe la sivyo athari zake zitakuwa kubwa.

Akizungumza katika kuadhimisha siku ya afya duniani yenye kauli mbiu kama hakuna hatua leo, basi hakuna tika kesho, mkurugenzi mkuu wa WHO Bi Margaret Chan amesema dunia iko katika hatihati ya kupoteza miujiza ya tiba kutokana na usugu wa dawa.

Ametoa wito kwa serikali, wataalamu wa afya, viwanda, jumuiya za kijamii na wagonjwa kuchukua hatua za haraka kupunguza kusambaa kwa usugu wa dawa, kudhibiti athari zake na kulinda madawa hayo kwa vizazi vijavyo

(SAUTI YA MARGARET CHAN)

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema usugu huo unachochewa na utumiaji uliosambaa wa madawa, kuyatumia kupita kiasi na kuyatumia vibaya. Ameonya kwamba usugu huo unaongeza gharama kubwa katika mfumo wa afya na kuleta athari kubwa katika maisha ya watu, ikiwa ni pamoja na kutishia kurudisha nyuma juhudi zilizopigwa katika kufikia malengo ya maendeleo ya milenia.

Siku ya kimataifa ya afya ambayo huadhimishwa kila mwaka imekuwa na hisia tofauti miongini mwa watu.

(MAONI AFYA TZ)