Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kushirikina na Mediteranian kunusuru misitu:FAO

UM kushirikina na Mediteranian kunusuru misitu:FAO

Katika juhudi za kuokoa misitu kwenye ukanda wa Mediteranian kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO limeanzisha ushirikiano ambao utakabili kitisho dhidi ya misitu na kutambua thamani yake.

Ushirika huo utaleta pamoja mashirika na taasisi 12 ikiwemo FAO na utajikita katika nchi sita za Kusini na Mashariki mwa Mediteraniani ambazo ni Morocco, Aljeria, Tunisia, Syria, Lebanon na Uturuki. FAO imetangaza ushirikiano huo katika kuadhimisha wiki ya pili ya mistu ya Mediteranian iliyozinduliwa mjini Avignon Ufaransa jana.

Bonde la Mediteranian linapoteza karibu ekari milioni moja za misitu kila mwaka kutokana na moto na kusababisha hasara za kiuchumi za takribani Euro bilioni moja.