Skip to main content

China yaadhimisha miaka 30 ya kulinda bayo-anuai

China yaadhimisha miaka 30 ya kulinda bayo-anuai

Huku China ikiwa ni makao ya jamii nyingi za wanyama na mimea ya mwituni pia imekuwa na wajibu mkubwa katika kulinda na kwenye matumizi ya bayo anuai duniani.

Miaka 30 iliyopita China ilikuwa ni nchi ya 63 kujiunga kwenye mkataba wa biashara ya kimataifa kuhusu jamii za wanyama na mimea ya asili iliyo kwenye hatari ya kuangamia .

Katibu mkuu kwenye mkataba wa biashara ya bayo anuai John Scanlon anasema kuwa lengo kuu ni kulinda jamii za mimea na wanyama zilizo kwenye hatari ya kuangamia na kuhakikisha kuwa biashara hiyo imesalia kuwa halali na inayotambulika.

Ameushukuru utawala wa China kutokana na wajibu ambao imetekeza katika masuala ya kutekekezwa kwa sheria , utafiti wa kisayansi na kwa kutoa hamasisho kwa umma.