Meya wa zamani wa Rwanda aenda jela maisha:ICTR

30 Machi 2011

Meya wa zamani wa Rwanda amekuhumiwa kwenda jela maisha kwa kushiriki kwenye mauaji ya kimbari nchini humo mwaka 1994.

Jean-Baptiste Gatete alikutwa na hatia na mahakama ya kimataifa ya kushughulikia mauaji ya kimbari ya Rwanda ICTR. Hatia hiyo ni ya mauaji ya mamia kama sio maelfu ya Watutsi waliokuwa wachache nchini Rwanda.

Wanyarwanda 800,000 waliuawa katika siku 100 za mauaji ya kimbari nchini humo. Mahakama ya ICTR iliyoko mjini Arusha Tanzania inaendesha kesi na kutoa hukumu kwa waliohusika na mauaji ya kimbari na makosa mengine ya ukiukwaji wa sheria za kimataifa za haki za binadmu yaliyotekelezwa nchini Rwanda.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter