Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wapongeza hatua za DRC kupambana na ubakaji

UM wapongeza hatua za DRC kupambana na ubakaji

Afisa wa Umoja wa Mataifa anayeongoza jitihada za kukabiliana na dhuluma za kimapenzi hii leo amekaraibisha hatua ya serikali ya Jamhufri ya kidemokrasi ya Congo ya kuwafungulia mashtaka maafisa wa ngazi za juu jeshini kwa kushutumiwa kuhusika kwenye vitendo vya ubakaji.

Kulingana na Margot Wallström mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya dhuluma za kimapenzi kwenye mizozo ni kuwa kati ya wanaofunguliwa mashtaka ni pamoja na jenerali Jerôme Kakwavu, luteni kanali Engagela pamoja na kanali Safari huku pia wawili zaidi wakitarajiwa kufunguliwa mashtaka kama hayo.

Bi Wallstrom anasema hatua hizi zinaashiria kuwa hakuna mwanajeshi au kiongozi wa kisiasa aliye juu ya sheria na pia hakuna mwanamke aliye chini ya sheria hiyo.