Juhudi kutokomeza ubakaji mpkani mwa DRC na Angola ziongezwe
UM yataka kuwepo juhudi zaidi kutokomeza vitendo vya ubakaji mpakani wa DRC na
Angola.
Huku kukiwa na ripoti za kufanyika kwa vitendo vya ubakaji kwa mamia ya wanawake ambao walikumbwa na vitendo hivyo wakati wakiwa njiani kurejea nyumba DRC toka Angola afisa wa ngazi za juu wa umoja wa mataifa anayehusika na matukio ya ubakaji kwenye maeneo yenye mizozo ametaka mamlaka za nchi zote mbili kuchunguza madai hayo na wakati huo huo kuchukua hatua za haraka kuzua kutotokea tena kwa
vitendo hivyo.
Mkuu huyo Margot Wallstrom amezitolea mwito mamlaka za pande zote mbili kuhakikisha zinawajibika kuwalinda na kuyatetea makundi ya kina mama ambayo mara kwa mara yanatumbukia mikononi mwa makundi ya kihalifu. Ripoti za hivi karibuni zinasema kuwa zaidi ya watu 12,000 raia wa Jamhuri ya Congo ambao walifukuzwa kutoka Angola kati ya Septemba na disemba mwaka uliopita wanadaiwa kwamba walikumbwa na matukio ya ubakaji.
Timu ya waangalizi wanaohusika na misaada ya usamaria mwema walipotembelea maeneo waliofikia wananchi hao wlaishuhudia matukio kadhaa ya kukatiza tama pamoja na kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji kijisnia. Mwezi uliopita Bi Margot alikutana na waathirika hao na kisha kufanya nao majadiliano na baadaye alielekea nchini Angola ambako alikutana na maafisa wa serikali