Haki za binadamu muhimu katika changamoto za Vietnam:UM

Haki za binadamu muhimu katika changamoto za Vietnam:UM

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu madeni ya nje na haki za binadamu Cephas Lumina amepongeza mfumo wa maendeleo wa Vietnam ambao unamuweka raia wa nchi hiyo kuwa kitovu cha maendeleo ya taifa.

Hata hivyo amesema mtazamo wa haki za binadamu unahitajika kushughulikia changamoto mpya zinazokabili maendeleo ya nchi hiyo.

Amesema ili kufanikisha lengo hilo ni muhimu sera za taifa za kiuchumi, kijamii na mipango ya maendeleo ikazingatia mfumo wa haki za binadamu ambao unahakikisha kuna uwazi, ushiriki na uwajibikaji kwa kila mtu. Bwana Lumina ameyasema hayo wakati akihitimisha ziara yake ya kwanza nchini Vietnam.