Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO inaendelea kuwahamisha majeruhi kutoka nchini Libya

WHO inaendelea kuwahamisha majeruhi kutoka nchini Libya

Shirika la afya duniani WHO kwa ushirikiano na wizara ya afya nchini Misri wanaendesha shughuli za kuwahamisha waliojeruhiwa kwenye mapigano yanayoendelea nchini libya ili wapate matibabau.

Majeruhi hao wanahamishwa kutoka mji wa Ajdabiya kwenda Benghazi huku walioko Beghazi wakihamishiwa Tobruk na Misri ili kuzuia msongamano kwenye mahospitali. Awali serikali ya Uturuki ilisema kuwa itatuma meli iliyo na magari ya kuwabeba wagonjwa na bidhaa za matibabu kwenda Libya ili kuwasafirisha raia 450 wa Libya waliojeruhiwa kupewa matibabui nchini Uturuki kama anavyoarifu Fadela Chaib kutoka WHO.

(SAUTI YA FADELA CHAIB)

WHO pia imebuni kituo cha kutoa mafunzo kwenye mji wa Tobruk ambapo wanaowahudumia wagonjwa wamekuwa wakipata mafunzo.