Skip to main content

Mkuu wa OCHA ahutubia mkutano wa kimataifa Dubai

Mkuu wa OCHA ahutubia mkutano wa kimataifa Dubai

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Valarie Amos leo amehutubia mkutano wa kimataifa wa msaada wa kibinadamu na maendeleo DIHAD 2011 mjini Duabai.

Mada kuu ya mkutano huo ni teknolojia mpya, na jinsi gani inavyoweza kuwa na athari katika operesheni za kibinadamu na maendeleo. Katika hotuba yake Bi Amos amesema katika dunia iliyozingirwa na taarifa moja ya changamoto kubwa ni kubaini zipi taarifa muhimu ili kusaidia kufanya maamuzi mazuri.

Ameongeza kuwa kuliko wakati mwingine wowote nguvu, rasilimali na juhudi za pamoja, zinahitajika ili kuimarisha uwezo wa kukabiliana na masuala ya dharura ya kibinadamu na msisitizo wa teknolojia mpya ni muafaka kabisa.

Bi Amos pia amekutana na Princess Haya Bint Al Hussein wa Jordan, mke wa Sheikh Mohammed Bin Rashid Al Maktoum, Makamu wa Rais na waziri mkuu wa Emarati na mtawala wa Dubai. Bi Amos ameushukuru uongozi wa kifalme wa Dubai kwa kuunga mkono na kujishughulisha na kuchagia katika masuala ya kibinadamu