Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji wa Kiafrika kutoka Libya wawasili Linosa Italia

Wahamiaji wa Kiafrika kutoka Libya wawasili Linosa Italia

Kundi la kwanza la wahamiaji wa Kiafrika karibu 830 kutoka Tripoli na Misurata Libya wamewasili kwenye kisiwa cha Linosa Italia kati ya Machi 26 na 28, na leo wanahamishiwa kwenye kisiwa cha Sicily nchini Italia.

Wengi wa wahamiaji hao ni kutoka Eritrea, Ethiopia, Sudan na Somalia, lakini pia kuna baadhi ambao wanatoka maeneo ya Kusini mwa Jangwa la Sahara. Hili ni kundi la kwanza la wahamiaji wanaokimbia Libya kuwasili Italia tangu kuzuka kwa machafuko nchini Libya zaidi ya mwezi mmoja uliopita.

Wafanyakazi wa shirika la Kimataifa la uhamiaji IOM wanasema wanawake 80 na watoto 12 ni miongoni mwa wahamiaji hao na mwanamke mmoja alijifungua kwa msaada wa wauguzi wa Italia akiwa katika msafara huo.

Afisa uhusiano na habari wa IOM Jumbe Omari Jumbe anafafanua ni kwa nini wameamua kuwapeleka Italia wahamiaji hao.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)