UM unawasaidia wakimbizi wasio na makazi Himalaya

UM unawasaidia wakimbizi wasio na makazi Himalaya

Umoja wa mataifa kwa kushirikiana na wabia wake wa maendeleo nchini Nepal wamechukua juhudi za haraka za utoaji wa misaada kwa familia 5,000 ambazo zimeachwa bila makazi mashariki mwa Himalaya baada ya kambi mbili zilitumika kuwahifadhia kuharibiwa na moto.

Kamishna wa umoja wa mataifa juu ya wakimbizi UNHCR nchini humo Stephane Jaquemet, amesema kuwa moto uliozuka hapo jumanne umeteketeza kambi mbili na kuharibu makazi mengine 700 ya wakimbizi.

Tayari kamati maalumu inayoratibiwa na serikali imeundwa ili kuanza kuchukua hatua za dharula kwa kushirikiana na mashirika ya umoja wa mataifa kufuatilia tatizo hilo. Taarifa nyingine zinasema kuwa kuna idadi kubwa ya wakimbizi kwenye maeneo hayo waliokosa makazi jambo linalozidisha changamoto kubwa.