Skip to main content

NGO's kuusaidia UM kupambana na mihadarati

NGO's kuusaidia UM kupambana na mihadarati

Mashirika yasiyo ya kiserikali yaani NGO\'s yako tayari kuusaidia Umoja wa Mataifa kupambana na tatizo la mihadarati.

Mkuu ya afisi ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na madawa ya kulevya na uhalifu UNDOC Yury Fedotov anasema kuwa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanatekeleza wajibu mkubwa katika kuusaidia Umoja wa Mataifa kupambana na tatizo la madawa ya kulevya kwa kuhakikisha kuwa wale walioathiriwa na madawa ya kulevya wamepata usaidizi wanao uhitaji.

Akiongea kwenye mkutano na karibu mashirika 100 yasiyokuwa ya kiserikali mjini Vienna Fedotov amesema kuwa jitihada zinastahili kufanywa ili kuzuia kuyategemea madawa ya kulevya na kuwapa matibabu wanaotumia madawa hayo.