Skip to main content

Baraza la haki za binadamu laafiki kuchukuza ukiukaji Iran

Baraza la haki za binadamu laafiki kuchukuza ukiukaji Iran

Baraza la haki za binadamu limekubaliana kuteuwa mchunguzi wa haki za binadamu kwa ajili ya Iran.

Azimio la kuanzisha mchunguzi limepitishwa kwa njia ya kura ambapo kura 22 zimeunga mkono, saba zimepinga na 14 hawakupiga kura. Azimio linaitaka Iran kushirikiana kikamilifu na mwakilishi maalumu na kuruhusu mwakilishi kuzuru nchi hiyo.

Marekani ni moja ya wajumbe wa baraza la haki za binadamu waliounga mkono azimio hilo, na mwakilishi wake ni balozi Eileen Donahoe.

(SAUTI YA EILEEN DONAHOE)

Iran imepinga hatua hiyo ikisema ni jaribio la kuvamia mfumo wa baraza la haki za binadamu kwa ajili ya kushughulikia nia za kisiasa za wajumbe wachache wa baraza hilo.