Skip to main content

Katika siku ya TB duniani, hatua zimepigwa lakini juhudi zaidi zinahitajika:UM

Katika siku ya TB duniani, hatua zimepigwa lakini juhudi zaidi zinahitajika:UM

Visa vya maradhi ya kifua kikuu kilichokuwa sugu dhidi ya tiba yanasababisha vifo 150,000 duniani kote kila mwaka na idadi inatarajiwa kuongezeka kwani kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huo kinapanda.

Shirika la afya duniani WHO limesema ifikapo 2015 kutakuwa na visa vipya milioni mbili vya waathirika wa kifua kikuu, idadi ambayo itakuwa imepanda sana ikilinganishwa na visa 440,000 vya mwaka 2009.

Katika siku hii ya kimataifa ya kifua kikuu Dr Peter Nunn wa WHO anasema ufadhili na tiba madhubuti vinahitajika kukabili ongezeko hilo.

(SAUTI YA DR PETER NUNN)

Naye mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Ukimwi UNAIDS Michel Sidibe katika ujumbe maalumu wa siku hii ya kifua kikuu amesema anatiwa moyo kuona ushirikiano wa mipango ya pamoja kupambana na ukimwi na kifua kikuu inaanza kuzaa matunda.

Amesema tangu mwaka 2002 kumekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wa TB ambapo pia wana virusi vya HIV. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)