Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bomu laua mmoja na kujeruhi zaidi ya 30 Jerusalem

Bomu laua mmoja na kujeruhi zaidi ya 30 Jerusalem

Bomu lililotegwa kwenye kituo cha basi kilichofurika umati wa watu limeripuka na kuua mtu mmoja na kujeruhi wengine zaidi ya 30 nchini Isarel.

Shambulio hilo la leo mjini Jerusalem ni la kwanza kushuhudiwa baada ya miaka kadhaa, na limetokea wakati ambapo mvutano na ghasia baina ya Israel na Palestina vikiongezeka.

Kwa mujibu wa Ray Dolphin anayefanya kazi kwenye ofisi ya kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA mjini Jerusalem anasema ni mara ya kwanza baada ya miaka mingi kutokea shambulio na anatumai kwamba huu sio mwanzo wa kuzorota kwa hali ya usalama.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali shambulio hilo na kusema ni kitendo kisichokubalika na kutoa wito wa kusitisha mara moja vitendo hivyo vya kigaidi dhidi ya raia ili kuzuia kupotea zaidi kwa maisha ya watu.