Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OCHA yatoa zaidi ya dola milioni 10 kusaidia Ivory Coast

OCHA yatoa zaidi ya dola milioni 10 kusaidia Ivory Coast

Shirika la Umoja wa Mataifa la kutoa ufadhili wa dharura CERF limetoa dola milioni 10.4 kwa mashirika saba yanayohudumu nchini Ivory Coast kusaidia kugharamia mahitaji ya kibinadamu nchini humo.

Mzozo wa kisiasa nchini Ivory Coast umesababisha madhara kote nchini hususan magharibi mwa nchin ambapo sekta za elimu na afya zimevurugika na karibu asilimia 90 wa wahudumu wa afya pamoja na idadi kubwa ya walimu wakiwa hawafiki kazini.

Uhaba wa madawa na bidha za kupima wagonjwa umezua wasi wasi wa kutokea kwa madhara ya kiafya kwa maelfu ya watu wanaoishi katika eneo hilo. Fedha hizo zitatumiwa kutoa huduma za afya , chakula, maji , usafi , elimu na kugharamia misaada mingine.