Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IAEA na FAO wazungumzia hofu ya mionzi ya nyuklia Japan

IAEA na FAO wazungumzia hofu ya mionzi ya nyuklia Japan

Shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA na shirika la chakula na kilimo FAO wametoa taarifa ya pamoja kuzungumzia ongezeko la hofu ya mionzi ya nyuklia na usalama wa chakula nchini Japan.

Taarifa yao imesema usalama wa chakula ni suala lingine linalohitaji kushughulikiwa haraka. Baadhi ya vyakula katika maeneo yenye mtambo wa nyuklia wa Fukushima Daiichi na maeneo ya jirani vimebainika kuwa na mionzi na hofu ya kusambaa mionzi ya nyuklia imeongezeka baada ya onyo la serikali kwamba maji ya bomba sasa sio salama kunywewa na watoto.

Serikali hata hivyo imesema inaendelea na jitihada zote kuhakikisha inadhibiti kusambaa kwa mionzi kwenye kinu cha nyuklia cha Fukushima Daiichi. Shirika la IAEA ambalo liko bega kwa began na serikali ya Japan kuhusu kusitisha athari za mionzi za kinu hicho limesema bila kuwepo kwa nishati ya umeme na mfumo wa kupoza mitambo sita ya kinu hicho hakitaweza kufanya kazi.

Limesema matatizo mengi katika kinu hicho yamesababishwa na kutokuwepo kwa umeme kutokana na tetemeko na tsunami hapo Machi 11.