Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji waendelea kusafirishwa baada ya IOM kupata fedha

Wahamiaji waendelea kusafirishwa baada ya IOM kupata fedha

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limesema linaendelea kusafirisha idadi kuBwa ya wahamiaji wanaokimbia machafuko nchini Libya baada ya kupata msaada wa fedha.

IOM ambayo imekuwa na vituo katika mpaka baina ya Libya na Misri na baina ya Libya na Tunisia kuwasaidia na kuwarejesha makwao maelfu ya wahamiaji tangu kuzuka kwa kitahanani nchini Libya mwezi uliopita lilikuwa na hofu ya kuendelea na operesheni zake kutokana na upungufu wa fedha.

Kama anavyofafanua afisa uhusiano wa habari wa IOM Jumbe Omari Jumbe baada kupokea msaada wa paundi milioni 4 kutoka shirika la Uingereza zitawasaidia kuendelea kutoa msaada.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)