Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi lazima liongezwe kukabiliana na TB duniani:WHO

Juhudi lazima liongezwe kukabiliana na TB duniani:WHO

Shirika la afya duani WHO, mfuko wa kimataifa wa kupambana na kifua kikuu, ukimwi na malaria na wadau wa kutokomeza kifua kikuu wametoa wito kwa viongozi wa dunia kuongeza juhudi za wajibu wao katika kufikia lengo la kuwapima na kuwatibu mamilioni ya watu wenye kifua kikuu kilichokuwa sugu dhidi ya madawa mchanganyiko (MDR-TB) kati ya mwaka huu 2011 na 2015.

Wito huo umo kwenye ripoti iliyotolewa leo na WHO iitwayo ‘kuelekea fursa kwa wote ya vipimo na matibabu ya kifua kikuu sugu ifikapo 2015". Ripoti hiyo inayoonyesha mafanikio kiasi katika baadhi ya nchi zilizo na mzigo mkubwa wa wagonjwa sugu wa kifua kikuu na imetoka siku moja kabla ya siku ya kimataifa ya kifua kikuu ambayo kila mwaka huadhimishwa Machi 24.

Mkurugenzi mkuu wa WHO anasema licha ya hatua zilizopigwa juhudi zaidi zinahitajika. Jason Nyakundi anaarifu.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Akifafanua kuhusu kukabili kifua kikuu Dr Mario Raviglione mkurugenzi wa WHO idara ya kutokomeza TB anasema mipango ipo lakini juhudi zaidi zinahitajika.

(CLIP OF DR MARIO RAVIGLIONE)