Hofu yawakumba wahamiaji wanaosubiri kusafirishwa Libya
Hali ya wasi wasi inazidi kuripotiwa baina ya maelfu ya wahamiaji waliokwama kwenye mpaka kati ya Libya na Tunisia wanaosubiri kuhamishwa.
Zaidi ya wahamiaji 22,000 kwa sasa huenda wako kwenye vituo vya Ras Adjir kwenye mpaka kati ya Tunisia na Libya au kwenye kituo cha Salum kwenye mpaka kati ya Misri na Libya.
Hata baada ya shirika la kimataifa la uhamiaji IOM , serikali kadhaa na shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa kusaidia takriban wahamiaji 30,000 kurejea nyumbani bado kutakuwa na mafanikio kidogo katika kupunguza idadi kubwa ya wakimbizi kwenye maeneo ya mipaka iwapo ufadhili wa dharura hautakuwepo.