Hali nchini Syria bado ni tete, huku maandamano yakiendelea

22 Machi 2011

Jumla ya watu sita wameripotiwa kuuawa na maafisa wa usalama siku ya Ijumaa kwenye mji ulio kusini mwa Syria Daraa baada ya maelfu ya watu kuingia mitaani kuandamana wakitaka kuwe na uhuru wa kisiasa na kumalizika kwa ufisadi.

Wakati wa maandamano hayo serikali ilijibu kwa kutumia vitoa machozi na maji na badaye kutumia risasi dhidi ya waandamanaji ambapo watu wanne waliuawa na wengine kujeruhiwa.

Kulingana na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ni kuwa siku ya Jumapili pia waandamanaji wengine waliingia mitaani kwenye mji huo wa Daraa ambapo maafisa wa usalama walijibu kwa kuwafyatulia risasi ambapo mtu mmoja aliuawa.

Ofisi hiyo ya Umoja wa Mataifa imelaani kuuawa kwa waandamanaji na kuitaka Syria kukoma kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter