Hakuna haja ya kuzuia watu kwenda Japan:WHO/WMO

Hakuna haja ya kuzuia watu kwenda Japan:WHO/WMO

Hakuna mipango ya mara moja ya kuweka vikwazo vya usafiri kuingia na kutoka Japan yamesema mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Shirika la afya duniani Who na lile la hali ya hewa WMO yanamtazamo kwamba kiwango cha mionzi mjini Tokyo na maeneo mengine ukiondoa yale yanayozunguka vinu vya nyuklia vilivyoharibiwa haijafikia kiwango cha kuweza kuchukuliwa kama ni tishio kwa afya ya jamii.

Mashirika hayo mawili yamesema kuwapima abiria wanaowasili kutoka Japan sio lazima. WHO pia imeuonya umma wa Japan dhidi ya kutumia tembe za potassium iodide au bidhaa zingine zilizo na madini hayo. Gregory Hartl ni kutoka WHO.

(SAUTI YA GREGORY HARTL)

Shirika la WMO linasema hali mbaya ya msimu wa baridi ambayo imekuwa kikwazo kwa shughuli za misaada ya dharura kwa waliokumbwa na tsunami nchini Japan inatarajiwa kupungua katika siku chache zijazo.