Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Liberia inahitaji msaada ikijiandaa kwa uchaguzi:UM

Liberia inahitaji msaada ikijiandaa kwa uchaguzi:UM

Afisa wa ngazi ya juu kwenye Umoja wa Mataifa amesema kuwa hata baada ya nchi ya Liberia kupiga hatua muhimu bado inahitaji kupewa uungwaji mkono wa kiamatifa wakati inapojiandaa kufanya uchaguzi na inapokabiliana na idadi kubwa ya wakimbizi kutoka Ivory Coast.

Ellen Margrethe Løj mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia UNMIL ameliambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuwa hali ya kisiasa na kiusalama kwenye taifa hilo la Afrika magharibi imekuwa ngumu kwa miezi ya hivi karibuni.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa umehudumu nchini Liberia tangu mwaka 2003 kusaidia kuupa nguvu mkataba uliomaliza mapigano yaliyodumu kwa miaka kumi ambapo karibu watu 150,000 waliuawa wengi wakiwa raia na kusababisha wengine 850,000 kukimbilia mataifa jirani.