Skip to main content

Mkutano wa UM waangazia zaidi uhusiano kati ya uhalifu na ugaidi

Mkutano wa UM waangazia zaidi uhusiano kati ya uhalifu na ugaidi

Afisa wa ngazi ya juu kwenye Umoja wa Mataifa amesema kuwa kunastahili kufanywa jitihada zaidi ili kukabiliana na vitendo vya uhalifu vinavyondelea kuongezeka duniani vikiwemo ulanguzi wa pesa na madawa ya kulevya pamoja na ugaidi. Mkutano huo ambao pia unashughulikia maslahi ya waathirwa wa ugaidi pia ulihutubiwa na mkurugenzi na pia mwanzilishi wa shirika Global Survivors Network Carie Lemack ambalo ni shirika lisilokuwa la kiserikali.

(SAUTI YA CARIE LEMACK)

Yury Fedotov mkurugenzi mkuu kwenye ofisi ya UM kuhusu madawa ya kulevya na uhalifu aliwaambia wanaohudhuria mkutano kuhusu ugaidi mjini Vienna kuwa faida inayotokana na shughuli za uhalifu inatumika kufadhili vitendo vya kigaidi.