Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP imeanza ujenzi wa kituo nchini Djibouti

WFP imeanza ujenzi wa kituo nchini Djibouti

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP leo limeanza kuweka msingi wa kituo chake kipya cha masuala ya kifundi nchini Djibouti ambacho kitatumika kama kiungo cha shirika hilo kwenye pembe ya Afrika.

Kituo hicho kitakachogharimu dola milioni 6, kinajengwa kwenye eneo la ukubwa wa mita 40,000 zilizotolewa na serikali ya Djibouti na kitakuwa na uwezo wa kuhifadhi tani 30,000 cha chakula.

Mkurugenzi wa masuala ya kiufundi wa WFP Martin Ohlsen amesema shirika lao linaamini kwamba kituo hicho kitarahisisha shughuli za msaada wa kibinadamu kuwafikia kwa wakati na gharama nafuu wanaouhitaji katika kanda hiyo.Djibouti inasalia kuwa na umuhimu mkubwa kwa WFP kwani inapitishia nchini humo msaada wa chakula kwenda Ethiopia na Somalia.

Hafla ya kuanza kwa ujenzi huo imeandalia na Rais Ismail Omar Guelleh wan chi hiyo, na kuhudhuriwa na maafisa mbalimbali wa serikali, jumuiya za kijamii, wawakilishi wa Umoja wa Mataifa na wahisani kutoka Djobouti na Ethiopia.