Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yatoa wito wa usafiri zaidi kwa wanaokimbia Libya

UNHCR yatoa wito wa usafiri zaidi kwa wanaokimbia Libya

Mkuu wa shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR António Guterres pamoja na katibu mkuu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM William Swing wamekamilisha ziara ya pamoja nchini Tunisia ambapo walihakikishiwa na serikali ya nchi hiyo kuwa mipaka yake itabaki wazi kwa wanaokimbia ghasia nchini Libya.

Kwa sasa kuna karibu watu 17,000 kwenye kituo cha Choucha kilicho kwenye mpaka waliko pia raia wa kigeni wengi kutoka nchini Bangladesh wanaosubiri kusafiri. UNHCR pamoja na IOM yanaendelea kutoa wito wa kutaka kutolewa usafiri zaidi kwa njia ya ndege kwenda nchini Bangladesh na nchi za bara Asia pamoja na za kusini mwa jangwa la sahara.

Hadi sasa zaidi ya watu 230,000 wametoroka ghasia nchini Libya wakiwemo watu 118,000 wanaokimbia kwenda nchini Tunisia , 107,000 kwenda Misri, 2000 kwenda Niger na 4300 kwenda nchini Algeria.