Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IAEA kuisaidia Japan baada ya kukumbwa na tetemeko

IAEA kuisaidia Japan baada ya kukumbwa na tetemeko

Shirika la kimataifa la nguvu za (IAEA) limetoa msaada kwa Japan ili kulinda mitambo yake ya nyuklia kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba nchi hiyo.

Hali ya tahadhari imetangazwa na shirika la nyuklia na usalama wa viwanda la Japan kwenye kinu cha Fukushima Daiichi ambacho kwa sasa kimefungwa.

IAEA imesema hadi sasa hakuna mionzi iliyovuja lakini mtambo umefungwa kwa ajili ya tahadhari. Serikali ya Japan pia imesema kumekuwa na moto katika kinu cha Onagawa ambao sasa umezimwa. Inakadiriwa kwamba nyuklia inatoa asilimia 30 ya nishati ya umeme nchini Japan.